GET /api/v0.1/hansard/entries/917536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 917536,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/917536/?format=api",
    "text_counter": 20,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii nichangie Ombi ambalo limeletwa na jirani yangu, Mhe. Caleb Amisi. Wakazi wengi wa Matisi ambao wako kando ya barabara wamejenga majumba ya biashara. Hao ni watu wenye biashara ndogo ndogo. KeNHA iliposema kuwa inataka kujenga barabara hiyo kutoka Kitale hadi Endebess mpaka kule Suam ili kutuunganisha na majirani zetu, ni vizuri waangalie malalamishi ya wakaazi. Serikali huwa na compulsory acquisition . Sio Matisi tu peke yake lakini ningependa Kamati inapoangalia, iangalie barabara hiyo kwa ujumla kwa sababu wako wakazi wa Endebess pia ambao wameathirika na ujenzi wa barabara hiyo. Barabara imepitia huko na hawako kwa orodha ambayo ilitolewa na KeNHA. Kwa hivyo, ninaungana na mwenzangu ili tufike mbele ya Kamati hiyo na watu wetu wa Matisi mpaka Endebess ili barabara ijengwe lakini wananchi pia wapate haki yao. Ahsante, Mhe Spika."
}