GET /api/v0.1/hansard/entries/918557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 918557,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/918557/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningetaka kujumuika na wewe kuwakaribisha wanafunzi wote walio katika Seneti yetu. Shule ya Msingi ya Kiwanja Ndege imebobea sana na tunatarajia kwamba itaenda mbali. Wamebobea na kuendelea kufanya vizuri. Wazazi pamoja na wanafunzi ni watu waliojitolea mhanga. Kwa hivyo, sisi tunawategemea wale wanafunzi na ninajua watakuwa viongozi wa kesho. Ninataka kuwaambia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kiwanja Ndege kwamba mmekuja hapa, mkaona vile ambavyo viongozi hapa Seneti wanavyojadili kwa weledi wa hali ya juu. Nawatakia kila la heri kwa masomo yenu. Muweke masomo mbele kwa sababu masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu. Bwana Naibu Spika wetu ambaye yuko hapa, ni mtu aliyebobea. Mkibobea mtakuwa Spika na hata Rais. Sisi tunawatakia kila la heri na mkirudi nyumbani msalimie wenzenu na muwaambie yale mliona. Asante."
}