GET /api/v0.1/hansard/entries/920307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 920307,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/920307/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ya taanzia kutoka kwa Seneta wa Vihiga kuhusiana na Marehemu Joe Kadenge. Kwanza ningependa kuchukua fursa hii kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya watu wa Kaunti ya Mombasa kupeleka rambi rambi zetu kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa mwendazake Kadenge kutokana na kifo chake hapo juzi. Joe Kadenge alikuwa mchezaji mpira mzuri, shupavu na vile vile aliiletea sifa nyingi nchi yetu ya Kenya. Kule Mombasa tuliweza kumtuza, ijapokuwa kwa uchache, mwendazake Kadenge na jina la barabara; ile barabara kuu inaoenda mpaka Stadium imeitwa jina lake ‘Joe Kadenge Street ‘. Kama tungekuwa na uwezo wa kufanya zaidi ya hapo, tungeweza kufanya. Kifo cha Kadenge, kinatupa nafasi ya kutafakari kama Taifa, ni mambo gani ambayo tunaeza kufanya katika nchi yetu ya Kenya ili kuhakikisha kwamba, mchezo inaweza kutiliwa maanani na vijana wetu ili wajiepushe na madhara ya madawa ya kulevya, itikadi kali na matatizo mengine ya jamii. Tukianza hapa katika Senate, utapata kwamba mambo ya michezo yamelumbukizwa pamoja kwa Kamati ya Labour, social relations, utamaduni, michezo, na mambo ya jinsia ambayo kwa hakika sio sawa. Ukiangalia mambo ya vijana, michezo na jinsia katika kila Kaunti, kila jambo inashughulikiwa na wizara kamili. Kwa hivyo hapa katika Bunge, tunapolumbukiza haya mambo yote pamoja inakua kwamba hatupati fursa kamili ya kutafakari mambo ya vijana na mambo ya michezo kwa ufasaha zaidi. Hii ni kwa sababu Kamati ya Labour inashughulikia mambo mengi kiasi ambacho haipati fursa ya kuweza kuangalia miradi gani wanaeza kusukuma hapa katika Bunge la Senate kuhakikisha kwamba vijana wanangaliwa Zaidi. Bi. Spika wa Muda, katika nchi yetu ya Kenya, kuwa mwanamchezo shupavu ni kwa juhudi yako mwenyewe. Hakuna taasisi yoyote ambayo inashughulikia kuwapea vijana fursa ya kuinua vipaji vyao vya michezo ili kuhakikisha ya kwamba michezo inakuwa katika kila eneo. Juzi, nilikuwa ninaangalia mchezo wa Tennis kule Wimbledon. Dada wa miaka 15 aliweza kumtoa Venus Williams katika raundi ya kwanza katika Tennis. Je, wasichana wetu hapa wanacheza michezo gani? Tukiangalia kila michezo, hivi sasa ni taaluma. Hii ni kwa sababu kila mchezo una wafadhili ambao wanasaidia kuhakikisha kwamba wanamichezo wanapata fedha na michezo hiyo inaendelea bora. Ukiangalia mchezo ambao unapendwa sana nchini Kenya, mchezo wa kandanda, hakuna shule za kandanda za Serikali ambazo tunawezapeleka vijana wetu. Mwaka wa 2013, Serikali ya Jubilee ilitoa ahadi kwamba itajenga stadium nane lakini mpaka leo hata moja haijajengwa. Je, wako kweli na nia ya kujenga michezo katika nchi yetu ya Kenya? Tukitafakari kifo cha Joe Kadenge, ningependa kusema kwamba jana tuliweza kumzika aliyekuwa referee maarufu ambaye alikuwa anaitwa Chiapo Ali Chiapo ambaye alikuwa referee wa kimataifa wa FIFA miaka 30 iliyopita. Tuliweza kumzika jana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}