GET /api/v0.1/hansard/entries/920308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 920308,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/920308/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mwingine ambaye tuko na yeye Mombasa ni Mzee Ali Kaja ambaye pia alikuwa mchezaji. Aliwahi kucheza mpira kwa timu ya taifa la Kenya pamoja na marehemu Joe Kadenge. Kwa hivyo tunapozungumzia kifo cha Joe Kadenge, tuzingatie kwamba kwa sasa kuna haja ya serikali kutilia mikazo zaidi maswala ya michezo kwa sababu michezo ndiyo inasaidia kukuza vipaji vya vijana wetu. Michezo kama riadha inapatia Kenya pesa nyingi kutokana na ushindi ambao huwa tunapata. Wanamichezo wengi wanapata shida kwa sababu hawajakuwa mentored . Hao hufikiria ya kwamba watazidi kupata pesa wanapozidi kukimbia na hiyo ndiyo huwafanya wajimalize kimchezo. Mbali na kujenga taasisi za michezo, kuna haja ya kuwekeza wataalam ambao watawasaidia wanamichezo ili tuweze kukuza taaluma zao kwa njia ambayo inakubalika kimataifa. Kuna haja sisi kama maseneta kuzingatia maswala ya michezo. Hii ni kwa sababu michezo inasaidia kupunguza maradhi, stress za kikazi na pia inatuwezesha kufanya kazi bila ya matatizo."
}