GET /api/v0.1/hansard/entries/922217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922217,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922217/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda. Najiunga na Hoja hii ambayo imeungwa mkono na wenzangu wote. Bubu ni mtu asiye na uwezo wa kuzungumza. Wakati unatesa bubu, itafika wakati bubu ataanza kububuja maneno ili aanze kuongea, unafaa kukimbia mbali sana. Tulikuwa tumenyamaza kwa muda mrefu sana, lakini sasa tunawaambia ndugu zetu kwamba hatunyamazi tena. Maseneta 52 walioandamana leo ni walinzi wa serikali za kaunti. Tulienda kortini leo kudai haki ya serikali za kaunti. Nia yetu ni kuona kwamba serikali za kaunti zimepata fedha zao na wanaweza kutekeleza wajibu wao kwa wananchi. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono kwa dhati Hoja hii na Jumanne ikifika---"
}