GET /api/v0.1/hansard/entries/922243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 922243,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922243/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kupunguza muda wa Mswada wa DORA ambayo imewasilishwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti. Kwanza, ninachukua fursa hii kuwapongeza viongozi, Spika na Maseneta wote ambao walijitolea asubuhi ya leo kufika mahakamani ili kuwasilisha kesi muhimu ambayo itaangalia mustakabali wa sheria kwa muda mrefu utakaofuata. Kilikuwa ni kitendo cha ujasiri na vile vile ni kitendo cha ustaarabu kwa sababu hatuwezi kuwa tunapigana saa zote wakati kuna taasisi za kisheria."
}