GET /api/v0.1/hansard/entries/922247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922247,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922247/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nimeona ya kwamba, ni kitendo cha ujasiri na pia cha kistaarabu kwa sababu sisi kama Wabunge hatufai kogombana hadharani kwa muda mrefu. Kilikuwa ni kitendo cha ujasiri na tunakiunga mkono na tutakuwa tayari sisi mawakili ambao tuko katika Bunge hili kuwakilisha kesi hii mpaka itakapofika tamati. Mswada ambao uko mbele yetu ni muhimu kwa sababu tumeona ya kwamba, DORA haijapitishwa, ilhali Bunge la Kitaifa lilipitisha Appropriations Bill . Inafaa tupitishe hiyo Division of Revenue Bill (DORA) kwa haraka zaidi ili kusiwe na upungufu wowote wa huduma kwa wananchi ambao wanategemea pesa hizi ziwafikie ili waweze kupata huduma mbali mbali kama afya na mengineo."
}