GET /api/v0.1/hansard/entries/922253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 922253,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922253/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii ya DORA. Ningependa pia kuweka sauti yangu katika kuheshimu Seneti kwa sababu tuko na nyumba mbili za kutengeneza sheria. Hasa Seneti hii inafanya watu ambao wametuchagua katika sehemu zetu kufikiwa na pesa. Kama kutakuwa na kizungumkuti cha watu ambao wanataka kupinga pesa zisifikie Wakenya, ni lazima sisi tusimame wima tuseme, hapana, haiwezekani. Ni lazima watu wetu wapate huduma za afya. Inafaa pesa zifike upande huo kwa sababu ikiwa pesa zitakuwa zinabaki hapa juu, tunajua hakuna maendeleo yatatendeka. Tuliapa kwa Biblia na Quran tukasema tutakinga ugatuzi kabisa usije ukaangushwa. Wale ambao wanapinga mambo ya Seneti ni wale wanaosema ugatuzi uanguke. Sisi tunasema ugatuzi uendelee na fedha zifike Mashinani. Pesa katika Mswada ambao ulikuwa umetolewa isipunguzwe hata kidogo kwa sababu Bunge la Kitaifa wanataka kupunguza fedha hizi, ila sijui ni wapi wanataka kuzipeleka. Sisi tuko wima, tumesismama kama milingoti kusema ugatuzi uendelee na pesa nyingi zifikie watu wetu ili waweze kupata huduma zile zinazofaa huko mashinani. Bw. Spika wa Muda mimi naunga---."
}