GET /api/v0.1/hansard/entries/922323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922323/?format=api",
"text_counter": 335,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Taarifa ya Sen. (Prof.) Kamar. Ninakotoka kuna mashamba makubwa ambapo mahindi yanakuzwa kwa wingi kupitia unyunyizaji maji. Kuna Hola, Bura na Galana-Kulalu irrigation schemes ambazo zinapatikana katika Kaunti ya Tana Rive. Nashangaa sana kusikia kuwa Serikali ina mpango wa kuagiza mahindi kutoka ng’ambo. Sehemu nilizotaja zinatosha kutoa chakula cha kutosha watu wa Tana River na Kenya nzima. Kwa nini tusikuze mahindi yetu hapa nchini badala ya kuagiza kutoka nje? Hilo ni swali ambalo tunafaa kujiuliza. Je, tuna upungufu gani? Tuna mito mikubwa ambayo ina maji kila wakati. Vile vile, tuna ardhi iliyo na rotuba. Jambo la kushangaza ni kuwa watu waishio karibu na mashamba ya kunyunyiziwa maji ndio maskini zaidi. Serikali haikuwezesha watu kupanda mahindi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}