GET /api/v0.1/hansard/entries/922324/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922324,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922324/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "katika sehemu za unyunyiziaji mashamba maji. Mashamba yetu hayanyunyiziwi maji jinsi inavyostahili. Ni kinaya kuwa Wizara ya Kilimo na Unyunyiziaji Maji haiwezi kusaidia watu wetu kupanda mahindi ili kupatikane chakula, kwa sababu nimeskia kuna mpango wa kuagiza chakula kutoka nchi nyingine. Tuna wataalamu, maji na ardhi bora ya kukuza mahindi. Nilishangaa kusikia kuwa maghala yetu yamejaa mahindi, lakini Serikali bado inapanga kuagiza mahindi kutoka nje. Hayo ni mahindi ambayo hatujui yanapandwa vipi. Pengine huwekwa dawa ambazo hazijulikani. Ikiwa tuna ardhi na maji ya kutosha, kwa nini tunawacha watu wetu kuteseka? Nafikiria tulienda na wewe kule Galana. Watu wa Galana ni maskini hohe hahe. Hata wamekatazwa kupeleka ng’ombe wao kunywa maji katika Mto Galana. Hii ni kwa sababu inasemekana kwamba sehemu hiyo ni ya irrigation. Imefanya watu wetu maskini na pia sisi hatuwezi kukipata chakula hicho. Kwa sababu hiyo, mimi naunga mkono Taarifa ambayo imetolewa na Sen. (Prof.) Kamar ili tuweze kutengeneza mambo. Kuna swali muhimu ambalo tunaweza kujiuliza. Kwa hivyo, nataka kumuachia dakika kidogo Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambaye yuko hapa nyuma yangu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}