GET /api/v0.1/hansard/entries/922402/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922402,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922402/?format=api",
"text_counter": 68,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kiswahili ni lugha ya taifa. Tunajua kwamba wengi wetu sio mahiri katika lugha hii. Lakini ni sawa kuwaruhusu Seneta wenzangu wazungumze lugha ya Kiswahili bila kutatizwa na hoja za nidhamu ambazo nyingine hazina msingi. Bw. Spika, ufasaha wa lugha unatokana na uzungumzaji wa lugha mara kwa mara. Kwa hivyo, nakubali kwamba ndugu yetu, Seneta, kutoka Gatuzi wa Narok hana uzoefu wa kuzungumza Lugha ya Kiswahili katika Bunge hili lakini akipewa fursa ataweza kuzungumza lugha hii kwa ufasaha kwa sababu alizaliwa kama Mmaasai na sio Mwingereza. Kawaida huwa anaongea lugha ya Kingereza kama Mwingereza. Asante sana, Mhe. Spika."
}