GET /api/v0.1/hansard/entries/922455/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 922455,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922455/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Ninaungana nawe kuwakaribisha wanafunzi waleo ambao umetaja kutoka kaunti za Makueni na Kajiado. Masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi yetu. Ni vizuri wamekuja kuona vile ambavyo tunajadili katika Seneti hii. Kuhusu kudhulumiwa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule zetu, si shida bali ni janga. Dhuluma hizi hutokea kila wakati na zimekuwa mazoea katika shule zetu. Tunataka Kamati ya Elimu ambayo itakashughulikia swala hili, iangalie kwa mapana na marefu, wakizingatia ya kwamba limekuwa likitendeka kila wakati. Wanafunzi wengi wameacha masomo yao kwa sababu wenzao wanawadhulumu ni kama wahuni na wakora. Kazi yao ni kudhulumiwa. Ni vizuri kama Kamati hii, iangalie mambo mengine ambayo yamekuwa yakijitokeza katika shule zetu. Kwa mfano, kuna swala la dawa za kulevya, pombe na kadhalika katika shule zetu za upili. Kamati isizingatie tu majukumu yale yalioyotajwa hapa, bali waangalie kwa mapana na marefu ili jambo hili likomeshwe mara moja. Kwa sababu ukiingia katika kidato cha kwanza, unapata mambo hayo yanaendelea. Shule zetu zimekuwa kama magereza ambapo wanafunzi hutezwa."
}