GET /api/v0.1/hansard/entries/922456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922456,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922456/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono taarifa hii. Tunaona ya kwamba watoto wakiwa wamekubaliwa kuingia shule za upili, hasa shule ambazo ni za hadhi ya juu, siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza au muhula wa kwanza, wanateswa na wenzao wa vidatu vingine. Wanaweza kuwafanya wenzao kuwa kama watumwa. Wakati mzazi anapopeleka mtoto wake shule, nia yake ni kwamba mtoto huyo aweze kujifunza na kupata masomo ambayo yatamfaidi siku zake za usoni. Lakini hii dhuluma inayoendelea katika shule zetu hakubaliki kamwe. Juzi tulisoma kwenye gazeti, jua ya Nairobi School ambapo wanafunzi wa kidatu cha kwanza walifanyiwa dhuluma kubwa na wenzao. Hii ni shule ya kifahari. Hayo ni makosa ambayo hatutaki yafanyike tena. Jambo hili hutokea kwa sababu walimu wamezembea kazini. Badala ya kuwafundisha watoto wetu, wao wanashughulika na mambo yao. Ni lazima wasomeshe watoto wetu ili wapate elimu ambayo itawafaidi katika masiha yao. Bw. Spika, vitendo hivi vinatendeka katika shule zetu za upili. Ninalikemea sana jambo hili la dhuluma katika shule zetu. Ni lazima tupate njia mwafaka ya kukomesha dhuluma katika shule zetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}