GET /api/v0.1/hansard/entries/922462/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922462,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922462/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Ahsante sana. Kuna kitendo cha kuzungumza na yule mtu ambaye anawapatia wenzake nafasi kuzungumza anaitwa “mzungumzishi”. Kwa hivyo, ninaweza kusema, Bwana Spika na katika hali ya kuunda Lugha ya Kiswahili, ninaweza iendeleza zaidi na kusema “Bwana Mzungumzishi”. Lakini, mtu ambaye anataka kutumia neno kama hili ni lazima azungumze kwa makini ndiposa maneno yasije yakamtatiza. Ukitaka kutumia neno “mzungumzishi”, ni lazima ujue kulitamka vizuri lakini pia unaweza kusema Bwana Spika. Ahsante tena, “Bwana Mzungumzishi”, kwa nafasi hii. Ninakuunga mkono kuwakaribisha wale ambao wamekuja kututembelea ili waone vile tunavyounda sheria katika Bunge hili. Jambo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni shida ambayo wanafunzi wetu wanapitia wakiwa shuleni. Watoto hawa hupelekwa shuleni kusoma ili wajiendelesha katika maisha. Lakini tunaona mara nyingi wakienda---"
}