GET /api/v0.1/hansard/entries/922470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 922470,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922470/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "Nimeangalia Katiba ya Kenya ambayo imeandikwa kwa Kiswahili na imechapishwa na Government Printer na hakuna jina “Mzungumzishi”. Nimeangalia pia nakala za Bunge na nimeona ya kwamba jina maalum la mtu ambaye anaongoza mazungumzo ya Bunge la Seneti ni Bwana Spika. Nimeangalia pia Kamusi na jina hilo halipo. Kiswahili cha watu wa Pemba ni tofauti na Kiswahili cha watu wa Mombasa. Kwa hivyo, hiyo Kiswahili ya dada yangu inaweza kuwa ile ya watu wa Kwale. Kulingana na Kiswahili sanifu ambayo inatumika katika Senate, wewe ni Bwana Spika na hauwezi kubandikwa jina nyingine."
}