GET /api/v0.1/hansard/entries/922480/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922480,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922480/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Hatufai kumsulubisha Sen. (Dr.) Zani kwa kutumia neno “mzungumzishi”. Hii ni kwa sababu lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inakuwa. Kwa mfano, katika msamiati au Kamusi ya Kiswahili hatukuwa na neno ‘tarakilishi.’ Lakini kwa vile lugha inaendelea kukua tumepata maneno mengi mapya. “Mzungumzishi” ni baadhi ya maneno ambayo yamekuja baada ya kukua kwa Lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, badala ya kumsulubisha Sen. (Dr.) Zani, angepewa muda wa kuwasilisha ushahidi kwamba neno hili linakubalika katika Lugha ya Kiswahili. Nafikiri hiyo ndio itakuwa njia sawa ya kumsaidia na kutusaidia sisi ambao tuko hapa. Lakini napinga ufafanuzi wa Sen. Wario kwamba “mzungumzishi” ni yule mtu ambaye anazungumzisha watu viziwi. Asante sana, Bw. Spika."
}