GET /api/v0.1/hansard/entries/922482/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 922482,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922482/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Pareno",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13180,
"legal_name": "Judith Ramaita Pareno",
"slug": "judith-ramaita-pareno"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ningemwomba dada yangu Sen. (Dr.) Zani alifutilie mbali neno “mzungumzishi”, kwa sababu halifai katika rekodi zetu za Seneti. Ni neno ambalo hatujui maana yake, kama vile tumeangalia katika Kamusi ya Kiswahili. Halifai kabisa. Bw. Spika, ningeomba pia kuwa kama wenzetu wanataka kuzungumza kwa Kiswahili, wanafaa kujifunza kwanza ili wasifanye Seneti kuwa mahali pa kujifunza."
}