GET /api/v0.1/hansard/entries/922491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 922491,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/922491/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13119,
        "legal_name": "Agnes Zani",
        "slug": "agnes-zani"
    },
    "content": "Asante sana. Kwanza, ningependa kusema kwamba katika Bunge la Kumi na Moja, swala hili liliulizwa. Sen. Kembi-Gitura alikuwa ameketi kwenye Kiti hicho. Tulilizungumzia na kukubali hili neno. Pili, katika hali ya kuendeleza lugha na falsafa ya lugha, ni muhimu kwamba lugha inaendelea kukuwa. Kama kuna wakati tunaweza kutumia jina lingine badala ya ‘Spika,’ ningefurahi sana, haswa sisi watu wa Pwani kama wakuza wa Lugha ya Kiswahili. Leo ningeskia wenzangu wakipiga makofi wakisema: “Leo umeleta neno jipya ambalo litatusaidia katika lugha.” Kuna wanafalsafa kama Prof. Abdul Aziz na Prof. Mberia kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi ambao tutazungumza nao. Sitaki kuwa na huzuni kwamba jina nzuri kama hili linaweza kuuliwa. Jina hili lilitumiwa katika Bunge la Kumi na Moja. Kwa hivyo, nikiendelea kuzumguza sitataja neno “mzungumzishi” na ‘Bw. Spika.’ Nitaendelea bila kutaja maneno yote mawili. Nikiendelea, tufikirie sana na wenzangu. Vile vile tunaweza kuwauliza wakuza lugha wengine watueleze kama “mzungumzishi” ni mtu ambaye anasaidia bubu kuzungumza. Je, bubu anaweza kusaidiwa kuzungumza? Bubu ni mtu ambaye hawezi kuzungumza. Kwa hivyo, ukisema unamfanya azungumze, unatuelezea nini hapa? Kwa sababu nafikiria nimewapa changamoto ya kufaa, namalizia nikisema kwamba ni muhimu walimu ambao wako katika shule hizi wawasaidie wanafunzi kama hawa ambao pengine wanapata shida tofauti tofauti. Tungependekeza kuwe na mwalimu maalum ambaye atakuwa anaweza kuchukua shida za wanafunzi na kuzitatua na kuhakikisha kwamba zimetatuliwa ili wanafunzi waendelee na mafunzo yao. Asante sana, “Bwana Mzungumzishi”."
}