GET /api/v0.1/hansard/entries/923643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 923643,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923643/?format=api",
    "text_counter": 32,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kuambatana na kifungu cha 47(1) cha Kanuni za Bunge la Seneti, nimesimama kutoa taarifa hii kuhusu mipango ya Serikali Kuu kujenga, kwa niaba ya kaunti tano za eneo la Pwani, makao makuu ya Idara ya Uvuvi katika eneo la South C, Jijini Nairobi. Bw. Spika wa Muda, kama unavyojua uvuvi ni mmojawapo ya huduma ambazo zimegatuliwa kuligana na Katiba ya Nchi. Huduma hizi, hivyo basi, zinapaswa kutolewa na Serikali za Kaunti, na maswala yote kuhusu uvuvi kusimamiwa na serikali zizo hizo. Kama inavyojulikana uvuvi unapatikana zaidi maeneo ya Pwani, maeneo ya Ziwa Victoria na Ziwa Turkana. Bw. Spika wa Muda, kuna mradi ambao unaitwa Kenya Marine Fisheries Social Economic Development Project ambao unasimamiwa na Kamati ya Blue Economy na Kenya Marine and Fisheries. Lengo na madhumuni ya mradi huu ni kuinua hali ya uchumi ya watu wa Pwani wanaohusika na uvuvi baharini, na pia kuboresha miundo msingi katika maeneo ya Pwani ili kuinua hali ya maisha ya wakazi wanaotegemea uvuvi baharini. Mradi huo unakusudiwa kufaidi kaunti tano, zikiwemo; Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River na Lamu. Mradi huo, unahusishwa na utafiti ambao utafanywa na taasisi ya “Kenya Marine and Fisheries”, ambayo, kama nilivyosema awali, makao yake yako Mombasa. Bw. Spika wa muda, jambo la kusikitisha ni kwamba hivi majuzi, Wizara ya Kilimo na Uvuvi imetangaza zabuni ya ujenzi wa makao makuu ya idara ya uvuvi,yaani Uvuvi House hapa jijini Nairobi. Ujenzi wa mradi huu unafanywa chini ya usimamizi wa Wizara ya Ukulima na Uvuvi kupitia, Taasisi ya Kenya Marine and Fisheries Institute ambayo makao makuu yake yako Jijini Mombasa. Ufadhili wa mradi huu unatoka kwa Benki ya Dunia. Kuwekwa kwa makao makuu haya Nairobi itakuwa ni hujuma dhidi ya ugatuzi, kwani maswali ya uvuvi yamegatuliwa kikamilifu katika katiba. Serikali inapaswa kulinda maeneo ya kuvua samaki ili yasiingiliwe na wavuvi wa kimataifa. Bw. Spika wa Muda, kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River na Lamu zina ardhi ya kutosha kujenga makao makuu hayo na wala sio Nairobi kwani itakuwa shida kwa wavuvi wahusika kuja Nairobi kutafuta leseni na mambo mengineo. Hakuna sababu yoyote ya kujenga makao hayo Nairobi kwa sababu uvuvi unafanyika Mombasa na maeneo mengine yaliokusudiwa na Benki Kuu ya Dunia ambayo ni; Kwale, Kilifi, Mombasa, Lamu na Tana River. Iwapo makao hayo yatajengwa Nairobi, itakuwa vigumu na gharama kuu kwa wavuvi kutoka, kwa mfano, Vanga, Kaunti ya Kwale, ama Kiunga- Kaunti ya Lamu, kusafiri hadi Nairobi ili wapate huduma katika ofisi za Uvuvi. Bw. Spika wa Muda, ninaiomba kamati husika ya Seneti ichunguze jambo hili ili kuhakisha kwamba Makao hayo yanajengwa Pwani kama ilivyokusudiwa na kwamba, kwa vile ni swala la uvuvi hizi kaunti tano zihusishwe kikamilifu. Asante sana, kwa kunipa fursa hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}