GET /api/v0.1/hansard/entries/923645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 923645,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923645/?format=api",
    "text_counter": 34,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, kama unavyojua, uvuvi hufanyika katika sehemu ya Bahari ya Hindi, huko katika Pwani ya Kenya hii, na pia katika maziwa makuu kama vile Ziwa Viktoria na Ziwa Turkana. Vile vile, uvuvi pia unafanyika katika mito mikuu, kama Mto Tana huko kwangu nyumbani. Bw. Spika wa Muda, makao makuu ambayo yatajengwa katika mji wa Nairobi, huko South C, hakika yatanyima utenda kazi, hasa zile stakabadhi zinazohitajika na wavuvi katika sehemu ya Pwani. Hii ni kwa sababu Benki ya Dunia ilitoa pesa hizi na hasa ikaangazia Tana River, Mombasa, Kwale na pia Lamu. Sehemu hizo ziko na ardhi ya kutosha kujenga makao makuu na ofisi zitakozotumika kufanya kazi hiyo. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, itakuwa dhuluma kubwa kwa watu kutoka Vanga huko mbali ya Pwani, hadi South C hapa Nairobi kuchukua vyeti vya uvuvi wa samaki. Wavuvi wa sehemu hizo ni masikini kabisa, na tukifanya hivyo basi tutawaongezea tena gharama ya kuja hadi Nairobi ili kupata stakabadhi muhimu za kuwawezesha kuvua samaki. Hivyo, hatutatawasaidia."
}