GET /api/v0.1/hansard/entries/923818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923818,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923818/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Ningependa kutoa maneno yangu kuhusiana na hii taarifa ambayo imeletwa hapa na Sen. Faki. Waswahili wanasema kwamba, ukishangaa ya Musa, nenda feri kule Likoni ndio utaona maajabu. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha katika historia ya nchi kuona Wizara nzima ambayo ina wasomi, wanaweza kufikiria kujenga makao makuu ya uvuvi, mahali kama Nairobi, South C, ilhali kuna kaunti tano za eneo la pwani ambazo ziko katika ufuo wa bahari na uvuvi wetu unaendelea huko."
}