GET /api/v0.1/hansard/entries/923828/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923828,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923828/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Spika Wa Muda, wenzangu wananisihi nizumgumze Kiswahili. Hawajui ya kwamba mimi ni gwiji katika mambo ya Kiswahili sanifu na hata utohozi, ufafanuzi na falsafa za Kiswahili. Mimi ni Seneta wa Kaunti ya Nairobi Mjini na ni kweli nimezaliwa mjini Nairobi. Wakati ambapo tulijaribu kuvua samaki, tulipata tu vyura wadogo au Tadpoles kwa Kiingereza, katika Mto Nairobi. Sen. Mutula Kilonzo Jnr. atakueleza ilikuwa hivyo katika Mto Kirichwa. Kwa kawaida, Seneta atasimama hapa kutetea jimbo lake kusema kwamba idara hii au taasisi fulani ibaki kwake. Lakini mimi kama Seneta wa Kaunti ya Nairobi Mjini, ninaienzi taifa letu, na pia ninaamini kwamba lazima tuwe na ugatuzi wa ukweli na haki. Wale ambao walifikiria kwamba wataleta ofisi ya halmashauri ya mambo ya uvuvi mjini Nairobi, nafikiri wamepotea kabisa. Nitaomba kwamba wafikirie tena. Tuna majimbo ambayo yana uvuvi katika eneo la Pwani kama vile wenzangu walivyosema. Tuko na uvuvi katika majimbo ya eneo la Ziwa Victoria; Kisumu, Migori na Siaya. Pia uvuvi unatendeka katika Kaunti ya Turkana. Kama kuna jambo ambalo lina umaarufu katika sehemu fulani kwa mfano, mambo ya kukuza majani chai, tuangalie majimbo ambayo yako katika maeneo ya majani chai. Kama ni mambo ya michezo kama vile mbio, tuangalie majimbo ya Nandi, West Pokot na Elgeyo-Marakwet. Bw. Spika wa Muda, Hii taarifa iliyoombwa na ndugu yangu, Seneta wa Kaunti ya Mombasa, haifuatilizwi kwa Kamati ya Bunge la Seneti. Kwa hivyo, ningemwomba ailete kwa njia mbadala. Akifanya hivyo, kama ni jambo la Kamati ya Ukulima, Ufugaji na Uvuvi, wataweza kualika Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ukulima na waseme kwa kinaga ubaga kile wanachojaribu kufanya. Asipofanya hivyo, itakuwa ni kama tu tumezungumza na tumepaka mafuta kwa mgongo wa chupa ama tumechezea mbuzi gita. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}