GET /api/v0.1/hansard/entries/923845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923845,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923845/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Pareno",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13180,
"legal_name": "Judith Ramaita Pareno",
"slug": "judith-ramaita-pareno"
},
"content": "Kuu ya Dunia, waliojitokeza na kuamua kufadhili mradi huo wa uvuvi katika Kaunti ya Kwale, Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu. Itakuwa maajabu iwapo Benki Kuu ya Dunia itajitokeza kufadhili kaunti tano ama kufadhili uvuvi na kuinua maisha ya wavuvi katika kaunti hizo tano, halafu Serikali ya Kitaifa iamue kwamba pesa hizo ambazo ni za wafadhili zitumike katika kujenga ofisi Nairobi. Kufanya hivyo, itakuwa ni kudhulumu wavuvi na haifai kabisa. Bw. Spika wa Muda, ingawa Katiba yetu imesema kwamba mambo ya uvuvi yako katika ofisi za kitaifa, basi ingefaa wale wanaopenda kujenga ofisi hizi za kitaifa hapa Nairobi watumie bajeti yao kufanya hivyo badala ya kutumia pesa za ufadhili, ambazo malengo yake yalikuwa ni kuinua wavuvi katika kaunti hizo nilizozitaja hapo awali."
}