GET /api/v0.1/hansard/entries/923850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 923850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923850/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Nikiongezea, Bw. Spika wa Muda, hivi sasa kuna kiwanda kikubwa cha samaki kinachojengwa na watu kutoka China katika sehemu za Shimoni. Samaki wanavuliwa, wanawekwa kwenye cold storage na kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Vile vile kuna miradi mingine inayoendelea sehemu za Shimoni, Mtwapa na Kilifi. I wapo wavuvi hawa kesho watakuwa na shida, watakimbilia ofisi gani? Hakuna ofisi nyingine, isipokuwa karibu ni pale sehemu za pwani. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Faki. Tunataka hii Kamati itakayohusika kuchunguza shida hii waangalie kabisa. Ilifikia vipi hadi uamuzi ukafanyika kwamba makao makuu yajengwe hapa Nairobi? Wanafaa waangalie kihaki kabisa, na watuonyeshe ilikuwa vipi Nairobi ikachaguliwa kama pahali patakapotengezwa makao hayo makuu. Bw. Spika wa Muda, sitaki kusema mengi, lakini naunga mkono hii taarifa iliyoletwa na Sen. Faki. Wale waliopanga njama ya kupendekeza makao haya yawe Nairobi, basi wajue kwamba ukweli utajulikana. Asante sana, Bw. Spika wa Muda. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}