GET /api/v0.1/hansard/entries/923860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923860,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923860/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, natakubaliana na Sen. Faki kwa sababu taarifa aliyoileta hapa ni wa maana kabisa. Ile tabu tuko nayo ni kuwa katika nchi hii, wakitaka kufanya kitu chochote, mahali pa kwanza wanapofikiria ni Nairobi. Nairobi imekuwa jangwa la ukuta. Kuna dunia nyingine iliyo na nafasi ya kutosha na wako na haki ya kuwa na makao makuu ya mradi wowote. Kama kila kitu kitafanywa hapa Nairobi, wale watu wengine wataenda wapi? Ni maajabu! Kwa mfano, wanasema mambo ya uvuvi yaletwe hapa Nairobi. Mambo ya wanyama wa pori yanataka kuletwa Nairobi. Kila kitu wakifikiria ni Nairobi. Hiyo haifai. Badala ya watu kusukumana hapa na pale, nafikiri huko kwetu, iwapo maji ya Tana River yatapelekwa upande wa Wajir, basi tutakuwa na ziwa kubwa sana. Pengine hata hili jangwa la ukuta lipelekwe huko Wajir badala ya kuletwa Nairobi."
}