GET /api/v0.1/hansard/entries/923868/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923868,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923868/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Hapo awali, ulitueleza kwamba kuna watoto kutoka Kajiado County ambao mpaka sasa wako pale juu. Nina kuunga mkono kwa kuwakaribisha kwa dhati. Ninawapa kongole walimu na watoto ambao wako katika madarasa ya chini kwa kuja katika Bunge la Seneti ili wasikie, watafakari na waoene Maseneta pamoja na Spika na vile tunafanya mambo yetu. Wao ni viongozi wa siku za usoni. Ninawapa changamoto ya kwamba hakuna lisilowezekana katika ndoto zao. Kama wanataka kuwa Maseneta siku moja, hiyo ndoto inawezekana. Kwa hivyo, wafanye bidii. Nimeketi katikati ya Maseneta wanaotoka katika kaunti za uchungaji. Shule hii ni moja wa shule nyingi inatoka katika sehemu za uchungaji. Upade wa kushoto niko na dadangu Sen. Pareno na upande wa kulia niko na kakangu, Sen. Olekina."
}