GET /api/v0.1/hansard/entries/923889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 923889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923889/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Kama kitu ni kizuri, kinakuja Nairobi. Mtu wa Kilifi akitaka msaada, atatoka Mombasa, Kilifi au Tana River mpaka Nairobi. Hiyo si ungwana. Maana ya ugatuzi ni nini ikiwa watu watatoka kule mashinani na kuja Nairobi? Watu wa chini wanafaa kufaidika na kuinuka kiuchumi. Kama ni nyumba za kupangisha, wale watakua maofisini wataenda kupangisha nyumba hizo na biashara itasongea. Ninaungana na wenzangu kwamba si haki zile ofisi zije Nairobi kwa sababu bahari iko Pwani. Ninauhakika watu kama wale wangepewe nafasi, wangehamisha bahari lakini Mwenyezi Mungu alipanga iwe kule. Wacha watu wa Pwani wafaidike na wale matunda yao. Mwenyezi Mungu aliwaumba na kuwaweka kule, kwa hivyo, wacha wale matunda yao."
}