GET /api/v0.1/hansard/entries/923890/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 923890,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/923890/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, shukrani kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia taarifa hii ya mipango ya Serikali Kuu kujenga kwa niaba ya kaunti tano. Sisi sote tunajua ya kwamba, kaunti hizi ni kaunti za uvuvi. Huu ni utendakazi ambao umegatuliwa. Katika serikali ya ugatuzi, ni lazima sisi kama Seneti ya Kenya tujaribu kuhakikisha ya kwamba, majukumu ambayo yamegatuliwa yafaidi wale watu walio katika kaunti. Tujenga makao haya hapa Nairobi ni madharau na upotuvu wa nidhamu na heshima kwa watu wa maeneo ya pwani. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Narok ninalipinga jambo hilo kabisa. Wakianza kuleta kila jukumu hapa Nairobi, kesho watasema kwamba ni lazima wajenge jumba kuu linaloshughulikia mambo kuhusu uuzaji na ununuzi wa nyama na ngano yote ambyo inatoka Narok hapa jijini. Tukikubali hayo yatendeke, tutakua tunafungua njia ya kaunti zetu zote kunyanyaswa na kufanywa kuwa maskini. Jambo hili ni dhuluma---"
}