GET /api/v0.1/hansard/entries/924153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 924153,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924153/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuwakaribisha wanafunzi kutoka Kaunti ya Bungoma. Ninawahimiza wanafunzi kwamba elimu ni msingi kwa maisha. Elimu ndio ufunguo wa maisha. Nawatakia kila la heri na kuwahimiza kutia bidii katika masomo yao. Kama wanafunzi hawa wanavyojua, Bungoma kumetoka watu mashuhuri sana. Spika wa sasa wa Seneti alikuwa gavana wa kwanza wa Kaunti ya Bungoma. Seneta Wetangula anayewakilisha Kaunti ya Bungoma pia ni Mbunge wa miaka mingi sana. Nawasihi wanafunzi watie bidii katika masomo na watii walimu wao kwani wao ndio viongozi wa kesho. Asante sana, Bw. Spika."
}