GET /api/v0.1/hansard/entries/924206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 924206,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924206/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukrani sana, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Mimi ningependa kuunga mkono taarifa hii inayohusika na mbuga za wanyama wa porini. Mimi natoka katika maeneo ya wakulima. Wakulima wa Mkongani, Magharini na Ganze wanaathirika wakati ndovu, twiga na wanyama wengine wanapovamia mashamba na kuharibu mimea yao. Bw. Spika, hii ni taarifa muhimu sana kwa watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama. Hivi sasa kuna hatari ya wawindaji haramu kumaliza wanyama wetu. Idadi ya ndovu na twiga imepungua sana. Haya yote yanaletwa na tamaa ya wawindaji haramu ambao wanawaua wanyama wetu. Naunga mkono taarifa hii ili shirika la KWS lipewe nguvu zaidi ya kuhakikisha wawindaji haramu hawapati nafasi ya kuwaua wanyama katika mbuga zetu hapa nchini. Ninaunga mkono Taarifa hii na kusisitiza ya kwamba ni lazima shirika linalohusika na mambo ya kulinda wanyama wetu lifanye bidii ili wawindaji bandia wasipewe nafasi ya kumaliza wanyama ambao wako na faida tofauti tofauti, kama vile utalii. Watu wanatoka sehemu mbalimbali kutalii. Hivi sasa, itakuwaje tunaweza kuwahesabu simba, ambao ni wanyama wanaosifika sana ndani ya msitu? Sijui kama waliobaki ni kumi au ishirini. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}