GET /api/v0.1/hansard/entries/924681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 924681,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924681/?format=api",
"text_counter": 558,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": ". Samahani Sen. Madzayo. Kama Kamati ya Uhasibu na Uwekezaji, tumeweza kuchunguza ripoti 235 za serikali za kaunti, ripoti 141 za mabunge ya kaunti, na zaidi ya ripoti 1,000 za hazina tofauti tofauti za serikali za kaunti, pamoja na mashirika ya kaunti kama vile mashirika ya maji. Kamati yetu pia ilichunguza hatari zote za kimaadili ambazo zinazikumba kaunti zetu ili kuangalia njia ya kuboresha utendakazi wa serikali za kaunti na mabunge yake. Hatari hizi zinaathiri pakubwa serikali za kaunti pamoja na mashirika ambayo yako chini ya kaunti hizo. Kuna hatari za kimaadili zinazohatarisha huduma katika kaunti zetu. Iwapo hazitachunguzwa na kutatuliwa, basi Seneti itapata shida kubwa. Shida hii itakuwa katika kuangalia ripoti za ukaguzi na hesabu za serikali za kaunti ili kuhakikisha kwamba usimamizi wa fedha unazingatia sheria na mwongozo ambao umewekwa. Bi. Spika wa Muda, Baadhi ya hatari mbali mbali ambazo zilijitokeza, mbali na zile ambazo Mwenyekiti wangu amezungumzia, ni kwamba kuna utaoaji wa zabuni ambao haufuati sheria. Zabuni nyingi zinatolewa kwa marafiki wa magavana, na viongozi wengine wa kaunti. Hiyo imaanisha kwamba kazi haitendwi vile inavyotakikana. Wakati zabuni zinatolewa kinyume na sheria, kuna miradi ghushi ambayo hutengewa pesa bila ya kutekelezwa na wanakandarasi. Vile vile, Bi. Spika wa Muda, kuna miradi ambayo huchukua miaka na mikaka kumalizwa. Hiyo inamaanisha kwamba wananchi hawapati matunda kutokana na rasilmali zinazotumika. Kwa mfano, katika Kaunti ya Kwale, kuna uwanja wa michezo ambao umekuwa ukijengwa kwa miaka sita sasa, na bado haujamalizika. Hiyo inamaanisha kwamba michezo ya kimataifa haiwezi kufanywa katika kaunti hiyo kwa sababu hakuna uwanja wa michezo hiyo kufanyika. Jambo linguine, Bi. Spika wa Muda, ni kuwa public participation pia imekuwa kizungumkuti katika kaunti hizi. Utapata kwamba marafiki na wapambe wa magavana, wabunge wa kaunti ama mawaziri katika serikali za kaunti ndio wanaitwa katika mikutano ya ushirikishi wa wananchi. Hiyo inamaanisha kwamba wananchi hawawezi kujua miradi ambayo inakusudiwa kufanywa katika maeneo yao. Vile vile hawawezi kukosoa makosa yanayotokea katika mikutano ama miradi ambayo inafanywa na kaunti zile. Bi. Spika wa Muda, pia kuna upungufu katika udhibiti wa ndani, yaani internal"
}