GET /api/v0.1/hansard/entries/924689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 924689,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924689/?format=api",
"text_counter": 566,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kwa Kingereza. Utapata kwamba wafanyikazi wengi wamekaa maofisini na hawafanyi kazi yoyote. Jana tulikuwa na Gavana wa Garissa, aliyesema kwamba yuko tayari kuchukua makarani waliokuwa wengi katika kaunti ile, ili waende wakafanye kazi kama waalimu wa shule za chekechea. Hicho ni kioja, kwa sababu karani ambaye amekaa ofisini hajui ni mambo gani yanayotakikana kufundishwa katika shule za chekechea. Pale ndipo panatikana msingi wa wanafunzi kufuata masomo kulingana na vile ambavyo anaweza kuelewa. Bi. Spika wa Muda, tatizo la uvimbe wa jopo la wafanyikazi linaathiri karibu kaunti zote. Vile vile, katika hao wafanyikazi, kuna ukosefu wa usalama wa kazi. Utapata kuwa gavana mpya akiingia ofisini, anataka kuja na wafanyakazi wake wote wapya. Hilo linamaanisha kwamba wale ambao walikuwa wameajiriwa mbeleni watapoteza kazi zao bila ya kuzingatia sheria. Kuwalipa itakuwa gharama kubwa, ambayo mara nyingi hupitishwa katika zile fedha ambazo zinatakikana kwenda katika miradi ya kusaidia kujenga kaunti zile. Bi. Spika wa Muda, kuna udhaifu katika usimamizi. Kamati za uhasibu zilizoanzishwa katika kaunti nyingi zimewekwa watu ambao hawawezi kuuliza maswali ambayo yanatakikana ili kuhakikisha kwamba kuna usawa na haki katika utendakazi wa kaunti hizi. Ina maana kwamba kamati za uhasibu katika kaunti nyingi zimeundwa kwa minajili tu ya kuonekana kwamba kuna kamati, lakini utendakazi wa kamati hizo haufai kuzungumziwa. Ripoti ambayo imeletwa katika Seneti hii ni muhimu sana katika kuhakikisa kwamba kaunti zetu zinaendesha kazi zake kulingana na sheria. Itahakikisha pia kuwa wananchi wanapata Huduma, kama ilivokusudiwa wakati ugatuzi ulipoanzishwa katika nchi yetu. Bila ya kuzingatia Ripoti hii, ina maana kwamba yale mambo yaliyofanyika katika miaka sita ya ugatuzi iliyopita yataendelea kufanyika. Hivyo basi, wananchi hawataweza kupata huduma kulingana na vile ilivyokusudiwa katika Katiba yetu."
}