GET /api/v0.1/hansard/entries/924885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 924885,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924885/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia hii Hoja ambayo imeletwa na mwenzangu, Mhe. Waluke. Ukiangalia hapa nchini Kenya, kile ambacho kinatufanya kila wakati tunaleta haya mambo wakati ambapo Serikali inaomba pesa nyingi kutoka nje, ama ile mikopo ambayo tunaagiza, ni kutotilia maanani zile kazi ambazo Wakenya wanafanya hapa na zile ambazo zinaweza kufaidi hii nchi kwa kuleta hela nyingi. Ukiangalia wakulima wa hili taifa la Kenya ni kama hilo suala limeachwa nje na Serikali ya Kenya. Utakuta zile bidhaa ambazo zinaagizwa kutoka kule nje ni bidhaa ambazo tunazitengeneza hapa nchini. Kama Serikali itayatilia maanani na kuanza kutilia mkazo zile bidhaa ambazo tunatengeneza hapa ni kumaanisha ya kwamba tutaweza kuwa na hela za kutosha na hatutaomba mikopo kutoka kule nje. Kwa mfano, kuna samaki ambaye tunamkuza katika nchi hii kule Kisumu na kule ambako wakulima wamewekeza na wanafanya kilimo cha samaki. Sio vizuri kuwa kila wakati tunaagiza samaki kutoka nchi ya China. Hiki ndicho kinafanya wakulima wa samaki kukosa matumaini ya kuendelea na hiki kilimo. Hiyo inapelekea nakisi kuendelea kuongezeka. Wakati ambapo Serikali inatenga zile fedha za kilimo, wakati mwingine unakuta wakati ambapo Bajeti inajadiliwa, hawatilii mkazo mambo ya kilimo. Kama wangetilia mkazo kilimo, tungekuwa tunakuza vitu vingi. Kama wakulima wa kahawa na wale ambao wanaweka mifugo, hizi ni bidhaa ambazo tungeziuza hapa nchini na kule nje na tupate hela. Pia wale wawekezaji ambao huwa wanakuja katika hili taifa kuwekeza, kama Serikali ingetilia mkazo na kuwahimiza ya kuwa hapa Kenya tuko na ardhi ya kutosha pale ambapo wanaweza kuja na kuwekeza vitu vyao, tungekuwa tunapata pesa nyingi kutokana na wale wawekezaji. Vile vile, katika zile jopo ambazo zinatengenezwa na Serikali kuenda kule nje kutafuta soko la bidhaa za hapa Kenya, ni vizuri wakati ambapo Serikali inafanya haya mambo, wakishirikiana na kamati za biashara pamoja na ukulima, waangalie kama yule mkulima wa miraa ameridhishwa. Pale natoka ile miraa tunakuza ni mingi sana. Wakati ambapo Serikali inaenda kule kutafuta soko, hakuna wakati ambapo nimesikia kuwa Serikali imeenda nje kutafuta soko la wakulima wa miraa. Saa zingine ile miraa tunauza kutoka kule ina hela nyingi. Wakati ambapo Serikali itajitolea na kuanza kutafutia pia wale wakulima wa miraa soko huko nje, inaweza kuleta pesa kwa wingi hapa na hakutakuwa na sababu ya kutafuta mikopo kule nje."
}