GET /api/v0.1/hansard/entries/924891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 924891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924891/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": "ya Israeli imeanza kununua ile miraa kutoka mwezi huu. Hizo ni pesa ambazo zitafaidi Serikali kwa njia kubwa. Ukiona zile bidhaa ambazo tunaagiza kutoka nje, ni bidhaa za hela nyingi ukilinganisha na zile ambazo sisi tunauza kule nje. Kwa hivyo, kama Serikali ingetilia mkazo wakulima wa hapa nchini, nadhani zile pesa ambazo tungekuwa tunaomba kutoka kule nje zingekuwa chache na mwananchi hangefinyiliwa na Serikali kwa kulipa kodi. Kwa hivyo, kile ambacho kinafanya wananchi walipe kodi ya juu ni Serikali imefeli kutekeleza yale ambayo yanaweza kumsaidia mwananchi katika kukuza bidhaa hapa ili tupate pesa nyingi. Wakati ambapo hii Hoja itapita, ni vizuri Serikali iangalie mwananchi kwanza, halafu yule ambaye tunanunua kutoka kwake awe wa pili. Hili litasaidia nchi kupata pesa kwa wingi. Sio vizuri wakati ambapo tuko na bidhaa ambazo tunaweza kuziekeza na zitoe pesa nyingi za kusaidia nchi, tunaweka mtu wa kutoka nje katika mstari wa mbele na kusahau watu wetu. Ni vizuri Serikali imshughulikie mwananchi wake kwanza kwa kuyashughulikia yale ambayo yanaweza kumsaidia kuzalisha fedha zaidi kushinda zile ambazo tunazipokea kutoka kule nje. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono. Asante."
}