GET /api/v0.1/hansard/entries/925346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 925346,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925346/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Huo ni mfano mmoja. Kuna wengine ambao wanaibiwa ardhi na mali zao bila kuhimili. Ukiwa na malipo ya uzeeni ambayo yanasimamiwa, inavyostahili, kama vile Mheshimiwa anavyopendekeza, kusikuwe na shida kama hizo. Maisha ya mtu anapostaafu yatakuwa na nafuu kwa sababu kuna senti ambazo atakuwa anategemea mara kwa mara kuliko hivi sasa ambapo watu wanastaafu na kungoja kwa miaka mingi sana bila kuona senti zozote na wanahangaika uzeeni. Ninamshukuru sana Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii muhimu. Ninamuunga mkono na ninashukuru sana kwa nafasi hii kwa mara ya pili."
}