GET /api/v0.1/hansard/entries/925581/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 925581,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925581/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Nimesimama hapa kuambatana na Kifungu 87 cha Kanuni za Bunge kinachohusu matumizi ya lugha bungeni. Lugha za matumizi katika Bunge la Seneti ni Kiingereza, Kiswahili na lugha ya Ishara. Order Paper, yaani karatasi hii kwa Kiswahili, ni chombo muhimu katika utaratibu wa maelezo ya yale ambayo yatatokea katika Bunge na hutolewa kila siku, masaa 12 kabla ya Bunge kukaa. Kwa hivyo, ni muhimu pia iandikwe kwa Lugha ya Kiswahili. Inapochapishwa kwa Lugha ya Kiswahili itawawezesha Wakenya wengi kufuatilia kwa ukaribu mazungumzo yanayoendelea hapa katika Bunge na pia kuwafahamisha yale ambayo yanajiri hapa. Bw. Spika, lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inakua. Kwa hivyo, tutapata fursa pia kuchangia katika kukua kwa Kiswahili na matumizi yake katika Bunge letu la Kenya na Wakenya kwa jumla. Nimefurahi kwamba wengi wa Maseneta wanaweza kuongea kwa Kiswahili sanifu. Leo tumeona mapema Seneta Maalumu, Sen. Omanga, akitoa mchango wake kwa Kiswahili bila shida yoyote. Kutafusiriwa kwa Order Paper hii katika Lugha la Kiswahili kutasaidia pakubwa wananchi pale nje ambao wanataka kufuatilia shughuli za Bunge hii kwa utaratibu kabisa."
}