GET /api/v0.1/hansard/entries/925582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 925582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925582/?format=api",
"text_counter": 231,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika. Nataka kumwunga mkono Sen. Faki kwa hoja hiyo muhimu sana. Karatasi hii ya utaratibu ambayo tunafanya hapa Seneti ni muhimu kwetu sisi na pia pale nje. Kuna watu wengi ambao wanafuatilia mambo ambayo tunafanya hapa. Wanataka kujua tunazungumza juu ya nini na vile ambavyo lugha yenyewe imetukuzwa na inaweza kuzungumzwa hapa. Kwa hivyo, ni muhimu karatasi hii iandikwe katika lugha ambayo inaweleweka na wengi wa Wakenya pale nje. Bw. Spika, ninamshukru sana kaka yangu kwa kuleta hoja hii. Ni muhimu kutafuta njia za kutekeleza mapendekezo haya."
}