GET /api/v0.1/hansard/entries/925583/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 925583,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925583/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. M. Kajwang’",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13162,
"legal_name": "Moses Otieno Kajwang'",
"slug": "moses-otieno-kajwang"
},
"content": "Bw. Spika, sisi kama wakaazi wa Homa Bay, na mimi kama kiongozi wao katika Bunge hili la Seneti, ningependa kumuunga mkono Seneta wa Kaunti ya Mombasa, Sen. Faki, katika hoja hii. Ni muhimu karatasi ambayo inapanga utaratibu wa Bunge hili la Seneti ichapishwe kwa Lugha ya Kiswahili. Ningependa kumwomba Sen. Faki, alete Hoja hapa Bungeni ili isiwe tu ni ile karatasi ya utaratibu lakini iwe pia ile ambayo tunaita Standing Orders kwa sababu imechapishwa kwa Lugha ya Kiingereza. Katiba inafaa ichapishwe kwa lugha ambayo Wakenya wengi wanaweza kuielewa. Wakati huu tunapozungumza, Katiba imechapishwa kwa lugha moja pekee. Isitoshe hata ripoti za kamati za Bunge hili hazifai kuchapishwa kwa lugha moja pekee. Tukipitisha Hoja kama hiyo, nina uhakika kwamba Maseneta na Wabunge watarudi shuleni ile wajifunze Kiswahili. Pia itabidi wanafanyikazi wa Bunge waimarishe uwezo wao wa kuandika ripoti kwa lugha ya Kiswahili. Bw. Spika, jambo hili ni la lazima katika Katiba yetu. Namuunga mkono, Sen. Faki."
}