GET /api/v0.1/hansard/entries/925589/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 925589,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925589/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hata mimi namunga mkono Seneta wa Mombasa kwa dhati. Ni kweli Katiba yetu imeorodhesha zile lugha ambazo za kutumika katika taifa letu; Kingereza, Kiswahili na pia lugha ya Ishara. Ukitamaza runinga hapa Bungeni ama wale ambao wanafuatilia shughuli zetu kule nyumbani kupitia runinga, hatuna yule ambaye anatafsiri kwa lugha ya ishara. Tungeomba pia jambo hilo liangaliwe kwa makini ili Wakenya wengi waweze kufuatilia yale ambayo tunafanya katika Bunge. Hii ni kwa sababu tunawakilisha majimbo na wale ambao wako chini kabisa, itakuwa bora tukijaribu kuzungumza Kiswahili siku moja kwa wiki kwa saa moja. Tunaweza kuamua iwe ni Alhamisi kati ya 2.30 p.m. na 3.30 p.m. ili pia kuwe na uzoefu kwa viongozi wetu kutumia lugha ya Kiswahili. Ninajua kuna wale ambao wako na changamoto, hasa wale ambao wanatoka karibu na Ziwa la Victoria. Wao husema Kiswahili, “Siyo mdomo chao”. Hata wanaisema vibaya lakini tunajua wakizaliwa wanaanza na Kiingereza. Hata watoto wao hulia kwa Kiingereza."
}