GET /api/v0.1/hansard/entries/925591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 925591,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925591/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Singependa jambo hili lichukuliwe juu juu. Nikitembea mitaania, kuna Wakenya ambao nimesikia wakisema kwamba wanamjua Sen. Faki na Sen. Madzayo huzungumza Kiswahili. Pia, wewe Seneta wa Nairobi, jaribu wakati mwingine kuongea Kiswahili. Ubaya wetu hatujaongeza sheng katika orodha ya lugha kwa sababu niko na vijana wengi sana ambao wanaielewa. Nimeona kwamba, wakati wenzetu wanajaribu kuzungumza Kiswahili, kuna hoja nyingi za nidhamu kwa sababu kile kiwango tumeweka Kiswahili kiwe sanifu si lazima. Wakati mwingine kuna utohozi wa lugha. Kuna maneno ambayo huwezi kutumia, labda utatumia tasifida ili watu waweze kuelewa na utumie maneno ambayo yanakubalika. Tusiwe wakali sana kwa kuangalia kanuni ama lugha iwe sanifu kama ya wale magwiji wa lugha. Tunataka iwe ni lugha ambayo watu wanaweza kuielewa na kujieleza kwa njia rahisi."
}