GET /api/v0.1/hansard/entries/925594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 925594,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925594/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13156,
        "legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
        "slug": "mutula-kilonzo-jnr"
    },
    "content": "Ninashangaa kwamba katika maeneo ambayo tumetoka kule nyumbani, wakati bunge za kaunti zinafanya public participation, wanazungumza kizungu na kuandika sheria kwa kizungu. Kwa hivyo, hawafuatilii mipangilio ya bajeti na miswada ambayo inafanywa, kama vile, Isiolo, Makueni, Kakamega, Siaya, Kisumu na kwingineko ambako hawana uzoefu wa kuzungumza Kiswahili. Wanapenda Kiingereza kuliko Kiswahili. Bw. Spika, inafaa tutafsiri Standing Orders kwa lugha ya Kiswahili. Katika talakilishi ambazo ziko mbele yetu, kutakuwa na orodha ya kazi ambayo tutaifanya kama vile Order Paper . Sen. M. Kajwang’ amesema, kwa umaarufu na umahiri tunauliza hoja iletwe ili tuweze kuiunga mkono na tupewe nafasi. Ninakumbuka utata wa ‘mzungumzishi’. Tupewe nafasi ya kuwa na Kamusi ili Sen. (Dr.) Zani akileta maneno ambayo ni ya kutubabaisha sisi ambao hatuzungumzi Kiswahil, tunaweza kumjibu kwa haraka."
}