GET /api/v0.1/hansard/entries/925596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 925596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/925596/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Asante sana, Bw.Spika. Ningependa kuunga mkono ndugu yangu Seneta wa Mombasa 001 kwa kuleta Hoja hii. Katika Kipengele cha 7 cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa Kingereza, Kiswahili na lugha ya ishara ni lugha za Bunge. Nakubaliana tuwe na taratibu ambayo imechapishwa kwa lugha ya Kiswahili na pia mfasiri wa ishara ili watu ambao hawawezi kusikia au kuzungumza waweza kupata nafasi ya kufuatilia yale ambayo yanajadiliwa katika Bunge la Seneti. Ninaunga mkono Seneta wa Makueni ambaye ni gavana mtarajiwa. Ameanza kujipigia debe kwa kusema kuwa wakilishi wa wadi wahakikishe yale yote wanafanya yanaandikwe kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni rahisi kwa wananchi kuelewa. Sisi kama Seneti, lazima tuchukue hatua hii ili Wakenya wote wa tabaka mbalimbali ambao hawajapata nafasi kuelewa Kingereza wapate nafasi ya kufuatilia yale mambo ambayo tunajadiliana hapa na kuhakikisha wanayaelewa. Wakati huu kuna mazungumzo ya kura ya maoni juu ya Katiba yetu hapa nchini. Ni vizuri Wakenya waweze kufuatilia mambo haya na kuyaelewa vilivyo. Jinsi ya kufanya hivyo ni kuhakikisha tumeiweka katika lugha inayoeleweka. Bw. Spika, katika Umoja wa Kimataifa, kuna watu ambao wameanzisha changamoto ya kuweka Kiswahili kama baadhi ya lugha ambayo itatumika. Kwa hivyo, ni lazima sisi kama Seneti kutoa huo mfano na tuhakikishe tumesukuma gurudumu la kuhakikisha kila mtu amezungumza, kuandika na kuelewa Kiswahili hapa nchini."
}