GET /api/v0.1/hansard/entries/92615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 92615,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92615/?format=api",
    "text_counter": 386,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. Kuhusu mambo ya wizi wa ng’ombe, ninamshukuru mwenyekiti wa Kamati hii kwa kuleta Hoja hii mbele ya Bunge. Jambo la wizi wa ng’ombe ni jambo ambalo lingeangaliwa kwa njia ambayo inaweza kusaidia wafugaji. Hili ni jambo ambalo limeleta hasara sana na tumepoteza watu wengi. Tumetembea Isiolo na Samburu East na tukaona chanzo cha shida hiyo. Mimi ninaona kwamba ingekuwa muhimu ili tutengeneze sheria ambayo itaweza kutatua shida hiyo. Tumeona mengi kule Isiolo na Samburu East. Hayo mambo yalikuwa yanafanyika hivi; vijana wakienda kuiba ng’ombe upande wa Samburu, upande wa Borana na Somalia pia watakuja kuiba. Kwa hivyo, kilikuwa ni kitendo cha kurudiwa. Watu wakiiba leo, wengine wanaenda kuiba kesho. Kwa hivyo, ingekuwa muhimu sheria ipitishwe ili ikomeshe wizi huo."
}