GET /api/v0.1/hansard/entries/926156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 926156,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/926156/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nizungumze juu ya Ripoti hii ambayo imeletwa na Kamati ya kusimamia Masuala ya Wanajeshi pamoja na Masuala ya Mambo ya Nje. Suala la ardhi ni jambo ambalo huleta hisia mbaya. Ni jambo ambalo limefanya watu kupigana ndugu kwa ndugu, kuumizana, kuuana na umwagikaji wa damu kwa sababu wenyeji wa kawaida wasipohusishwa vizuri, bila shaka ni jambo ambalo linaweza kuleta utata mkubwa sana. Nikiangalia Ripoti hii, Kamati imefanya kazi lakini sioni kama wameimaliza kazi yenyewe vizuri. Wangehusisha viongozi wote kama viongozi wa kaunti na wa Bunge ili waafikiane na wananchi kuhusu njia mwafaka ya kufanya kazi hii. Jambo ambalo ni wazi ni kuwa Wizara ya Ulinzi wa Nchi inayosimamia masuala ya wanajeshi hapa nchini inahitaji ardhi upande wa Narok. Lakini juu ya kuhitaji ardhi upande wa Narok, ni lazima waipate kwa njia ambayo ni sawa na ya uwazi. Nikiangalia mapendekezo ya Kamati hii pale mwisho yananitatiza mno. Hii ni kwa sababu waliolalamika walipoona kuwa tangu pale mwanzo kulikuwa na mchezo fulani uliochezwa, basi wangependekeza kuwa Tume ya Kusimamia Masuala Ya Ufisadi na yule anayesimamia suala la uhalifu hapa nchini, haswa, Director of Criminal Investigations (DCI), waangalie ni jambo gani lililoendelea. Lakini kabla wafikie hapo, nina imani kuwa wangekuwa wamezungumza na viongozi wote kwa jumla na kuhakikisha kuwa wananchi ambao ni wahusika kwenye kipande hiki cha ardhi, wacha hawa wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}