GET /api/v0.1/hansard/entries/92621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 92621,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92621/?format=api",
    "text_counter": 392,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningeomba unisaidie niseme machache tu. Wakati hao ng’ombe walichukuliwa, hawakuchunguza kama walikuwa wametokana na wizi ama ni wa mama maskini ambaye hana kitu kingine, ama ni wa mzee ambaye mtoto wake hakuwa ameenda kuiba. Hao ng’ombe walikusanywa na watu kupatiwa. Sasa utashangaa ni kwa nini wasifuate wezi mpaka mahali wameenda. Kwa sababu hao wezi hawatoki nchi nyingine bali ni sehemu hiyo tu. Kwa hivyo, ingechunguzwa ili ijulikane wizi umetoka wapi na wezi wafuatwe. Ninawashukuru vijana wetu kwa sababu wamesema kwamba wanataka kazi. Mimi ningeomba kwamba hao vijana wapewe kazi. Hiyo ndio shida iliyoko katika jamii ya wafugaji. Vijana hawana kazi. Ningependekeza kwamba vijana waajiriwe kama askari kwa sababu wanajua kutumia bunduki. Kwa sababu ya ujuzi wa kutumia bunduki ni afadhali wawekwe katika mpaka ili wauchunge mpaka wa Kenya. Kwa hivyo, ninaomba Serikali ichukuwe hatua ya kupatia hawa vijana kazi ya kuchunga mpaka wa Kenya badala ya kupeleka watu ambao hawawezi hiyo kazi. Ni afadhali wapeleke vijana wa Samburu na Turkana huko."
}