GET /api/v0.1/hansard/entries/926323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 926323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/926323/?format=api",
"text_counter": 20,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": " Mheshimiwa Spika, naunga mkono haya malalamishi. Tusiongee sana kuhusu masuala ya mpaka lakini inadhihirika hata wakati wa uchaguzi kuwa watu wa Mtito Andei hawampigii kura Mheshimiwa Jessica Mbalu, wanampigia kura Mbunge wa Voi anayeitwa Bwana Jones Mlolwa. Tusiendelee kuongea zaidi kuhusu hilo suala maanake kuna makamishna ambao wanahusishwa na hayo. Kwa kweli, hili suala la wanyama ni swala tata na sugu. Nimelalamikia suala hili kwa muda mrefu. Nilichangia asilimia kuu katika ile sheria ya kulinda wanyamapori ya mwaka 2016. Lakini ninashangaa kuwa masuala ya kulipa wananchi ambao mimea yao imeharibiwa na wanyama au kujeruhiwa hayajatekelezwa mpaka leo. Ningeomba Kamati yetu Tekelezi ifuatilie hili suala. Kule kwangu Taita Taveta, watu wangu wamefukarika kwa sababu ya wanyamapori. Watu wangu wana bidii, wanafanya shughuli za ukulima, wanafuga wanyama, lakini bahati mbaya wakati hao ndovu, simba na wanyamapori wengine wakija kwa maeneo ya binadamu, wanatufanyia uharibifu mkubwa sana. Mheshimwa Spika, kuna wakati hata wewe mwenyewe uliagiza kwamba shughuli hii ifanyike kabla ya siku 60. Nashukuru kuwa KWS ilianza kutengeneza ua ambao ndio suluhu ya kila kitu. Lakini kwa bahati mbaya, lile ua walikuwa wanatengeneza lilikuwa linapitia kwa mashamba ya wananchi badala…"
}