GET /api/v0.1/hansard/entries/926816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 926816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/926816/?format=api",
    "text_counter": 62,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Bw. Spika, kama unavyojua, katika nchi yetu hii ya Kenya, mara nyingi sana katika uteuzi wa kazi huwa zina shida sana. Kusema kweli, Mheshimiwa Malalah hii Taarifa uliyoleta Seneti siku ya leo itakapojadiliwa na Kamati hii, itatoa mambo mengi sana. Hii ni kwa sababu umesema unataka kujua ni mabalozi na wakurugenzi wangapi ili tuweze kuhakikisha haki inatendeka. Bw. Spika, hatusemi kwa ubaya kwamba kuna ubaguzi. Kama unavyojua, sisi ni watu wa nchi moja na tunapendana. Hata hivyo, wakati wa ugavi wa kazi, utashangaa. Wala sitaki kusema mengi. Kamati ambayo itateuliwa ichunguze jambo hili, itatoa ukweli na tutajua ni watu gani waliopewa nafasi hii."
}