GET /api/v0.1/hansard/entries/926904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 926904,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/926904/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13175,
"legal_name": "Millicent Omanga",
"slug": "millicent-omanga"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu kwa niaba yangu, familia yangu na Wananairobi kwa jumla kuomboleza mhe. Ken Okoth, Mbunge wa Kibra na Bi. Gavana wa Kaunti ya Bomet. Kusema kweli ugonjwa wa saratani umetunyang’anya watu waadilifu. Kama wenzangu walivyosema, mhe. Ken Okoth ambaye alikuwa kijana na kiongozi hapa Nairobi kwa miaka yake michache, kama Mbunge wa Kibra, alifanya mengi. Aliyekuwa Mbunge kabla yake, akawa Waziri Mkuu na akawa Mbunge miaka 20 hakuweza kufanya yale mhe. Okoth alifanya kwa miaka saba ambayo alikuwa Mbunge. Bi Gavana ambaye ametuacha amekuwa mama ambaye ni kioo kwa sisi akina mama uongozini. Ni mama aliyetuonyesha mwelekeo. Pia aliweza kutusaidia sisi akina mama ambao tumeingia uongozini."
}