GET /api/v0.1/hansard/entries/926914/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 926914,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/926914/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Bw. Spika, sikusema kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu hakufanya kazi yoyote. Nilikuwa ninazungumzia kilio change na vile ninaweza kuomboleza kama Sen. Omanga. Nazungumza kama mkaazi wa Nairobi kuwa marehemu Ken Okoth amefanya kazi nyingi kwa miaka tano ambayo haikufanywa hapo awali. Tuko na mama na watoto wetu ambao wanaishi Kibra. Kwa hivyo, sisi kama wakaazi wa Kibra tunasema kuwa marehemu alisaidia kujenga mashule ambayo hayakuwa kabla yeye kuingia uongozini. Sijasema kuwa aliyemtangulia hakufanya chochote. Nilisema kwa maoni yangu na maombolezi yangu kwamba huyu kiongozi ambaye ametuwacha alifanya mengi kuliko ambayo tulifanyiwa miaka 25 iliyopita. Ningependa kuomboleza na kutoa majonzi yangu kwa hao waheshimwa wawili ambao wametuacha. Tunafaa tutafute tiba ya huu ugonjwa wa saratani. Pia ningependa tuweke mikakati ya kuwezesha watu wetu kupimwa ili ugunduliwe kabla ugonjwa huu haujaingia kwa mwili sana. Pia tunafaa tutoe mafunzo kwa wananchi jinsi wanafaa kuishi na kula ili kuzuia kupata saratani. Ningehimiza idara za Serikali ambazo zimeidhinishwa kuangalia vyakula kama nyama na vyakula vingine, wachunguze hivi vyakula kwa makini sana."
}