GET /api/v0.1/hansard/entries/927000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927000,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927000/?format=api",
    "text_counter": 246,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu ambao unataka kufanya mageuzi katika sheria zetu zilizoko za ugonjwa wa saratani na vile tunaweza kujikinga ili tusipatikane na athari zake. Tangu tuingie hapa mwaka 2017, tumempoteza Seneta mmoja, ndugu yetu, Seneta wa Migori aliyeshikwa na ugonjwa wa saratani ya koo na kupoteza maisha yake. Ikiwa itawezekana, ni muhimu kusisitiza zaidi kwamba Serikali iweze kuchukua hatua na iweze kuweka kipaombele na uangaliwe sana kama janga la kitaifa. Watu wanaofariki kutokana na athari za ugonjwa wa saratani ni wengi sana. Si wa Bomet, Elgeyo Marakwet ama sehemu za Rift Valley tu, bali Wakenya wengi wanapoteza maisha yao kwa saratani. Hata kule Kilifi Referral Hospital kuona wadi maalum ya wagonjwa wa saratani. Tunajiuliza maswali mengi. Tangu tupake Uhuru, hatujawahi kuwa na visa vingi vya ugonjwa was saratani kama ilivyo sasa. Namshukuru ndugu yangu, Sen. (Dr.) Ali, kwa kuleta mageuzi katika sheria ya ugonjwa wa saratani na vile mtu anaweza kujikinga ili kufanya maisha ya Wakenya yawe bora zaidi. Nikiangalia uzuri wa Mswada huu ni kuwa kila kaunti ya Kenya itatakikana kuwa na cancer centre, ambayo itakuwa katika hospitali na kila mtu atapewa nafasi ya kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa saratani. Hilo ni jambo nzuri. Ni lazima tulisisitize vifaa hivi vyakuchunguza ugonjwa viwe katika kila kauti hapa nchini. Bw. Naibu Spika, Wakenya wengi wamepoteza pesa nyingi wakitafuta matibabu ya wapendwa wao. Watu wameuza nyumba wanamoishi, mifugo, mali zao zote na vitu vyote ndani ya ili baba, mama, shangazi, nyanya au ndugu zao waweze kupona kutokana na ugonjwa huu wa saratani. Hatima ya kufanya hivyo, watu wao wanafariki. Mfano mzuri ni huu wa dada yangu, Dr. Laboso, aliyepata tabu sana. Alienda hospitali Ulaya na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}